12/02/2023
DINI ZILIVYODIDIMIZA MAENDELEO YA FIKRA NA UCHUMI BARANI AFRIKA.
SEHEMU YA 1.
Kabla sijaanza kuandika makala hii naomba kuwatahadharisha wasomaji na watakaopenda kufuatilia Makala hizi,kwamba chochote ninachoandika hakilengi kuleta uchochezi wa Tamaduni,Dini au imani fulani,.Hivyo nawasihi hata wasomaji na wachangiaji kufuata utaratibu wa kutokiuka mipaka ya ukosoaji.
Makala hii inaandikwa na Mtu mwenye uelewa wa kawaida wa kibinadamu na utimamu wa akili ,Na hata haya ninayoyaandika yanatokana pia na ufahamu wa watu wengine waliotangulia ukihusisha na historia ya nchi yetu, bara la Afrika na duniani kote.
Tuendelee..............
DINI
Dini ni Mkusanyiko wa imani, desturi, na mifumo iliyopangwa ambayo mara nyingi inahusiana na imani na ibada ya nguvu zinazotawala, k**a vile Mungu wa kibinafsi au kiumbe mwingine asiye wa kawaida. Dini mara nyingi huhusisha imani za kitamaduni, mitazamo ya ulimwengu, maandiko, unabii, mafunuo na maadili ambayo yana maana ya kiroho kwa washiriki wa imani fulani, na inaweza kujumuisha mazoea mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mahubiri, matambiko, maombi, kutafakari, mahali patakatifu, alama, mawazo, na karamu.
Hiyo ni tafsiri ya kawaida ya mazingira ya dini zilizopo katika jamii zetu,Lakini dini zinaweza kutafsiriwa tofauti kwa kila mmoja kutokana na kile anachokiamini(Imani)kupitia dini au mafunzo mbalimbali ya kiimani.
Duniani kuna dini nyingi sana na zote zina asili yake k**a.sio chimbuko lake.japo ni dini chache ambazo zina wafuasi wengi na zinatambulika zaidi.Baadhi ya dini zitambulikazo duniani ni pamoja na
1.Ukristo
2.Uislamu
3.Uyahudi
4.Uhindu
5.Ubuddha
6.Dini za Jadi za Kiafrika.
Ukristo ndio Dini inayotajwa kuwa na wafuasi wengi na yenye ushawishi mkubwa kutokana na historia yake na ueneaji wake.Uislamu unafuatia pia .
Ukristo uko Afrika katika wingi wa madhehebu yaliyopatikana katika historia ya Kanisa, baadhi katika bara hilo, baadhi katika mabara mengine.
Kwa sasa ndiyo dini kubwa zaidi barani Afrika, hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Uislamu ambao unaongoza Kaskazini kwa jangwa hilo(chanzo cha kifungu hiki ni (sw.m.wikipedia.org)
Na dini hizo mbili ambazo zimeenea zaidi barani Afrika zimeletwa na Wazungu (Ukristo) na waarabu (uislamu).
Na hili linathibishwa na historia ya Afrika hasa ukanda wa mashariki kabla na baada ya ukoloni,ambapo kulikuwa na Misafara ya Wazungu waliotoka ulaya na waarabu waliotoka Asia kufanya tafiti mbalimbali na Ufanyaji biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa.
KABLA NA BAADA YA UKOLONI
Waafrika kabla ya kuja waarabu, wareno , waingereza, waberigiji, wafaransa, wahindi na wachina. waliamini uwepo wa mungu ila swala lilikuja pale pa kumwaabudia huyo Mungu.
Nini maana halisi ya neno "Mzimu"?
Mzimu ni marehemu, ambapo Kiafrika kiasili tuliamini kuwa wafu wapo karibu na Mungu hivyo tulikuwa tunaomba mizimu itusaidie maana wao wapo karibu na Mungu. Ni sawa na Wakatoliki wanavyoamini katika Saints.
lakini kwenye dunia ya leo tunaamini
"Maana ya neno "Mzimu", ni Mashetani ambao ndio humuongoza kufanya maasi, wakati mtu anakata roho hao Mashetani hutoka, hao ndio "Mizimu". Mizimu ni Mashetani walio toka kwa WAFU, kutii Mizimu ni kutii Mashetani, na si kutii WAFU."
Ila ukweli wa mambo ni kuwa neno SHETANI sio neno lenye asili ya kiafrica . Concept ya shetani imeletwa afrika. waafrika walikuwa hawaamini uwepo wa shetani.
Mzimu imefananishwa na shetani baada ya dini za kigeni kufika afrika ila
imani ya uwepo wa shetani imeletwa hapo mwanzo haikuwepo.
Waafrika wengi wanaamini mababu zetu hawakuamini Mungu bali mizimu. Kumbe sio kweli Mungu alikuwepo ila tuliamini ndugu zetu waliokufa walikuwa wanatuunganisha sisi na Mungu, hivyo ili maombi yako yafanikiwe unaongea na mizimu (marehemu wa ukoo wenu).
Waafrika tuliamini Mungu, ila tukaamini Mungu yuko karibu na wafu (mizimu/mababu na ndugu walokufa) ambao tuliamini wanaishi katika mibuyu na miti nk. Sio kwamba tuliabudu miti
Ndio maana dini za Kiafrika hazikuwa na wamisionari wa kusambaza kwasababu, kila mtu aliomba Mungu kupitia mizimu ya ukoo wao. Mizimu ya ukoo wa mwezako ulikuwa hakusaidii hivyo hakukuwa haja ya kusambaza dini za asili, kila mtu aliomba kikwao.
Ila watu weupe ndio wakatufunza kuwa Mungu kwa imani zetu sio sahihi. Kwahiyo wasingekuwa wao bado tungeamini Mungu kinamna yetu.Mawazo ya ALLY NASSOR PX(JamiiForum).
KWANINI DINI ZIMECHANGIA KUDIDIMIA KWA MAENDELEO YA FIKRA NA UCHUMI BARANI AFRIKA?
K**a kumbukumbu ziko sawa kabla Wakoloni hawajaanza kutawala barani Afrika ,walituma vitangulizi vyao vya kuja kuchunguza bara la Afrika ambao ni
1.Wapelelezi
Hawa walikuwa
Ja kwaajili ya kujifunza jiografia ya Afrika ,Tamaduni za waafrika nk.Lengo lilikuwa ni kuwarahisishia wakoloni watakapokuja waweze kujua wanaanza na mambo gani.
2.Wafanyabiashara
Hawa walikuja kuangalia soko la bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ulaya ambazo zingefaa kwa kuwauzia Waafrika ,na pia ilikuwa ni njia ya kuchukua mali za waafrika Kirahisi kwa kubadilisha na bidhaa zao feki zilizchakatwa viwandani.
3.Wamissionari
Hawa ni watangulizi waliokuja Afrika kwa mgongo wa Dini.na hawa ndio na waona ilikuwa ni nguzo kubwa sana ya ukoloni kwa sababu kwa asilimia kubwa ni k**a walikuja kuaandaa mazingira ya kufikia wakoloni.
Na udhaifu wa kutumia dini kujiimarisha kiutawala ndio ulianzia hapa,Unajua ni kwa sababu gani?
_Wakoloni wengi walianza kuingia Afrika Mashariki inasadikika walikuwa wakifikia kwenye Nyumba za wamissionari na baadhi tu ya watemi waliokuwa ni vibaraka wa ukoloni kwa wakati huo.
_Wammissionari walianzisha shule mbalimbali na waliruhusu waafrika wachache kusoma humo na misingi mikuu waliyoilenga kwenye elimu hiyo ni masuala ya dini.ambayo dini hiyo baadaye ilitumika k**a ushawishi wa kukaribisha wageni ambao ndio wakoloni.
Lakini pia Shule hizo zilitumika k**a motisha kwa wakoloni waliotumwa kutawala Afrika kwa kuwasomesha watoto wao ambao kimsingi ilitakiwa wapate elimu huko kwao.
_Maeneo mengi ambayo wamissionari walijenga makanisa au shule ,ni yale maeneo ambayo yalikuwa na mali nyingi k**a madini na maeneo ambayo yalikuwa karibu na vyanzo vya uchumi k**a mito ,maziwa na bahari.
Na katika hili k**a serikali zetu huru zitaamua kujikita kwenye uchunguzi wa kina kwenye maeneo ambayo makanisa ya zamani yalijengwa basi naamini kwa kiwango kikubwa watapata siri kubwa ya yale yaliyojificha.
Mpaka leo tunapozungumza makanisa mengi au baadhi ya dini zinaendelea kutumia mgongo wa ufadhili ili hali katika maeneo wanayofadhili kuna kitu bado wanakitafuta wafadhili hao.
Kuna kanisa moja huko karibu na kijijini kwetu kuna mzungu mmoja ambaye alienda kwa jina la ufadhili kwenye kanisa moja ,inasemekana aliomba kuwachimbia washarika choo cha kisasa,ila aliomba serikali na waumini wa kanisa hilo wampe ridhaa ya kuchimba pasipo kuingiliwa na mtu yeyote.Alipopewa ridhaa ya kuendelea inasemekana alichimba shimo refu sana lisilo la kawaida kwa vyoo ,na alikuwa akichimba usiku na siku moja muumini mmoja aliyekuwa karibu na huyo Mfadhili alimuona akitoka na kitu fulani ,sasa kutokana na uelewa mdogo wa yule muumini hakufuatilia na kwa maelezo inaonekana ilikuwa ni madini.
Baada ya mzungu yule kupata alichokitaka aliaga na kuahidi angerudi kuja kumalizia ujenzi wa vyoo vya kisasa ,tokea hapo sasa ni karibu mwaka wa kumi hajawahi kuja Tanzania na mawasiliano yalikatika na kuwaacha watu wakihuzunika na shimo kubwa lililokuwa likitishia usalama wa watoto na wazee(Chanzo cha hadithi hii ni Mzee mmoja wa kijijini kwetu)
Itaendelea,,,,